Kwa
mujibu wa Mulokozi, (1996) anaeleza dhana ya fasihi kwa upana kuwa, huko ulaya
dhana hii imekuwa ikihusishwa na neno la Kilatini “Literra” ambalo lina maana
ya “herufi “au “uandikaji”. Neno la Kiingereza “Literature” limechipuka
kutokana na neno hilo la kilatini.
Wamitila,
( 2013:3) anaifafanua fasihi kwa maana
finyu na pana, Anasema kuwa katika ufafanuzi wa fasihi kuna utata wa neno
lenyewe fasihi. Aghalabu,
tunapoitumia maana hii huwa tunajenga maana yake finyu kurejelea utanzu
kama mashairi, tamthiliya , riwaya na
hadithi fupi. Katika maana yake pana anasema kuwa ni jumla ya insha fulani, hotuba, matini , vibonzo au
katuni na hata filamu.
Stella,(
2015: 17) anasema Fasihi ni taaluma ya sanaa ya lugha, yenye ubunifu ndani
yake, na inayo fikisha ujumbe kwa hadhira kwa kutumia njia ya maandishi au kwa njia ya mdomo.
Kwa
mtazamo wangu , nawezakusema kuwa Fasihi ni
ujuzi wa kutumia sanaaa ya lugha
iliyobuniwa kwa lengo la kufikisha ujumbe
kwa hadhira kwa kutumia njia ya maaandishi au njia ya mdomo.
Ni
kweli dhima ya fasihi hujifungamanisha na mazingira ya mwandishi lakini si kwa
mazingira ya mwandishi pekee, bali kwa jamii nzima itakayofikiwa na kazi
husika. Hivyo basi, kwa muktadha huo tutangalia
ni kwa jinsi gani dhima za fasihi
hujifungamanisha na mazingira kama
ifuatavyo;
Kuelimisha,
kazi ya fasihi hulenga kuelimisha jamii kwani dhana ya kuelimisha ndiyo chachu
ya maendeleo katika jamii, hasa katika kujikomboa kutoka chini ya utawala wa
ukandamizaji na utawala wa kinyonyaji au usiofaa. Mfano; katika tamthiliya ya
“Kivuli Kinaishi” ya Mohammed, (1990: 128) anasema;
Sauti
Nyingi; ( kutoka nje ambako zinajongea
ndani) “Sisi ni vizazi vipya vya Giningi, vizazi vya walioangamia,,,Ni vizazi
vya walio didimia, Sisi sasa tuna kinywa
kipana, tunauwezo wa kuamua
tunavyotaka,,,, kuamua wenyewe,,, kwa masrahi ya sote,,, hatutachagizwa tena na
uchawi, tunakuja ,,,tunakuja.”
Dhima
ya kifalsafa, huelezea vipengele mbalimbali kuhusu maisha ya watu katika jamii.
Waandishi husema kuwa palipo na mvutano
wa wema na ubaya lazima wema ushinde,
hivyo haki hutendeka . Dhana hii inajidhihirisha katika jamii yeyote ile, kwani
kila jamii inahitaji haki, ili iweze kujenga jamii yenye usawa na demokrasia. Dhana hii imejitokeza katika tamthiliya ya Kivuli
Kinaishi ya Mohammed, (1990:128) ambapo,
mwandishi ananukuliwa akisema,
Macho
ya Bi Kirembwe; ( sauti ya macho
inaonekana inatoka mbali); Mimi ni shahidi wa maovu yote uliyoyatenda ya kudidimiza
na kuangamiza.(Bi Kirembwe kwa kuchechemea);Hata macho yangu leo
yanasema.
Dhima
ya kiitikadi, Hii ni dhima ambayo inategemea muktadha wa jamii husika, nafasi
ya mtunzi na msimamo wakewe kulingana na matatizo na migogoro ya wakati wake
katika jamii husika. Mzingira (Mandhari), mwandishi huchukua kazi yake katika
mazingira yanayo mzunguka au jamii iliyo mzunguka kwa ujumla wake, kulingana na ujumbe
alioukusudia kwa jamii yake. Mfano; Katika riwaya ya “Barua Ndefu kama hii”ya
Marium Ba, (1994:103) anasema ;
“Kwa maoni yangu, uvaaji wa suruali ulikuwa
unatisha, kama mtu hukuwa na unene uliozidi ka ma ule wa kina mama wa
kimagharibi.”
Dhima
ya kiuchumi, uchumi ni pamoja na kuhamasisha uzalishaji mali, na kuongeza
kipato kupitia shughuli za kiuchumi na
kijamii. Uchumi wa jamii hukua endapo kama kutakuwepo na uongozi bora katika
jamii, yaani unapinga rushwa na unyonyaji. Katika tamthiliya ya “Kivuli
Kinaishi” mwandishi amejadili kwa upana katika (Uk; 24- 25) kwa kumtumia mhusika;
Bawabu II ambaye anapokea rushwa kutoka kwa mfanya biashara, kitu ambacho kinarudisha
nyuma maendeleo ya kiuchumi na kinaondoa usawa katika jamii ya Giningi.
Dhima
ya kisiasa, dhamira hii inadokezwa na waandishi wengi, kwani ni suala ambalo
huwezi kulitenga na maisha ya mwandishi na jamii yake kwa ujumla, Kwa mfano;
harakati hisi za kisiasa wakati wa ukoloni, zilikuwepo kwasababu rasilimali nyingi ziliibiwa na wakoloni kwa
ajili ya kuimarisha miradi yao, ilihali, viwanda vidogo vidogo vya Waafrika
vikididimizwa na wakoloni hawa. Mwandishi wa “Barua Ndefu kama hii” katika (Uk;
25) anasema;
“Je ilikuwa sawa kwetu sisi kufurahia utelekezwaji wa viwanda vidogo vidogo vya
uhunzi, ufundi wowote ule na ushonaji viatu?”
Dhima
ya utamaduni, katika utamaduni; fasihi
inamajukumu ambayo ni pamoja na
kuhifadhi na kurithisha amali za jamii, kuburudisha ,kuhasa, na
kulekebisha jamii. Kazi yeyote ya fasihi uhusishwa moja kwa moja na utamaduni, kwani mwandishi huchota maudhui( dhamira) yake kwa
kuzingatia dhana ya utamaduni wa jamii husika, iliyomzunguka na tamaduni
zingine za ki- ulimwengu katika kuonesha uhalisia wa kile kinachoelezwa na
mwandishi. Kwa mfano; Katika Tamthiliya ya “Kivuli Kinaishi”
mwandishi ameonesha mambo ya kiutamaduni
kama vile Matumizi Ya Ngoma, Kuwalisha unga wa Ndere na unga wa rutuba.
Mwandishi ametumia Ngoma za ki-utamaduni katika (UK. 48) Anasema;
“Ngoma inasikika tena
kwa mpigo mmoja mmoja, pole pole na taratibu na wote ispokuwa wazee wanacheza
na halafu gafla inasita”
Hivyo
basi, Fasihi inajifungamanisha na jamii yake lakini sio tu mazingira ya
mwandishi pekee, bali kwa kuangalia mazingira kwa ujumla wake kijiografia na
kiutamaduni.
MAREJELEO
Marium
Ba, (1994) Barua Ndefu Kama hii.
Mkuki na Nyota publisher. Dar es Salam
Mulokozi,
M .M (1996) Utangulizi wa Fasihi ya
Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam.
Mohammed,
S (1990) Kivuli Kinaishi. Oxford University
Press; East Africa Ltd: Kenya.
Stella,
F (2015) Fasihi ya Kiswahili, Ushairi,
Tamthiliya, na Riwaya. KiberaSeaboys General Interprises.Dodoma.
Hongera kwa kazi nzuri๐๐
JibuFutaKiswahili kitukuzwe
JibuFutaKazi nzuri sana
JibuFuta